Hadithi
Ngano
hadithi za kimapokeo amabazo hutumia wahusika kueleza au kuonya kuhusu maisha
Sifa za mtambaji
-anapaswa kuwa na ubunifu -anafaa kujua hadhira yake na mahitaji yake -anafaa kuielewa lugha ya hadhira yake -anafaa kuyaelewa mazingira ya hadhira yake -anapaswa kuwa jasiri -anafaa kujua utamaduni wa hadhira yake -anafaa kuwa mfaraguzi -anafaa kuwa mcheshi -anastahili kuwa mbaraza anayeingiliana vyema na watu
fomyula katika ngano
-fomyula ya ufunguzi -fomyula ya kuhitimisha -matumizi ya balagha -matumizi ya nyimbo -matumizi ya usemi halisi
Vipera vya hadithi
-hadithi za kubuni -hadithi za kisalua/ kihistoria
Umuhimu wa fomyula wa kuhitimisha
-huashiria mwisho wa ngano -hutangaza funzo kwa wasikilizaji -baadhi huwapa wasikilizaji changamoto ya kuwa watambaji mashuhuri wa ngano -humpisha mtambaji afuataye -hutoa hadhira kwenye ulimwengu wa ubunifu na kuiashiria kuw imerudishwa kwenye ulimwengu halisi -ni kitulizo kwa hadhira ambayo iliacha kuwa makini
Majukumu ya hadithi
-huelekeza jamii dhidi ya uovu -hurithisha elimu ya jamii -hukuza uwezo wa kukumbuka -huhalalisha baadhi ya desturi za jamii -huonya, huelekeza, hushauri, huadibu na kunasihi jamii -huhifadhi na kuendeleza historia ya jamii -kitambulisho cha jamii -hukuza ujasiri wa kuzungumza hadharani -huliwaza na kuburudisha baada ya shughuli za kazi -hukuza ubunifu -huunganisha watu katika jamii
Umuhimu wa fomyula ya ufunguzi
-huvuta makini wa hadhira -huashiria mwanzo wa hadithi -huweka mpaka kati ya ulimwengu halisi na wa hadithi -hushirikisha hadhira na mtambaji
Sifa za ngano
-huwa na fomyula maalum -usimulizi wake huwa na urudiaji -huwa na wahusika wa aina nyingi -huwa na matumizi ya nyimbo -ploti huwa sahili -hadithi za mafunzo -huwa na matumizi mengi ya fantasia -huwa na motifu ya safari -huwa na upenyezi wa mtambaji -matukio hayajikiti katika kipindi maalum
sifa za hadithi
-huwa na wahusika -huwa na ploti sahihi -hutumia lugha nathari -huwa na fanani -kwa kawaida hutambwa jioni baada ya shuguli za mchana -huwasilishwa kwa hadhira hai -huwa na mahali maalum pa kutambia -lazima iwe na mgogoro -baadhi huwa na fomyula maalum za ufunguzi na kumalizia
Umuhimu wa matumizi ya nyimbo
-kushirikisha hadhira -kuangazia maudhui makuu -kutoa ukinaifu -kuzindua waliolala
Umuhimu wa matumizi ya usemi halisi
-kutoa uhalisia katika hadithi -kuweka ladha katika utambaji
Nafasi ya mtambaji katika uwasilishaji wa hadithi
-ni mhusika mshiriki -ni msanii
Hadithi
masimulizi yanayowakilishwa kwa lugha nathari kuhusu watu, matukio na mahali mbalimbali